Back to News

TAARIFA YA FURSA YA KUSHIRIKI MAONESHO YA JUA KALI / NGUVU KAZI YA EAC🔥🔥

10 Nov 2025
TAARIFA YA FURSA YA KUSHIRIKI MAONESHO YA JUA KALI / NGUVU KAZI YA EAC🔥🔥

Ndugu Wanachama TWCC1,

Tunapenda kuwataarifu kuwa usajili wa kushiriki Maonesho ya 25 ya Juakali / Nguvu Kazi ya Afrika Mashariki (EAC MSMEs Trade Fair) umefunguliwa rasmi. Maonesho haya makubwa yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 1 hadi 10 Novemba, 2025 jijini Nairobi, Kenya.

Kwa wanachama watakaopenda kushiriki Maonesho haya hakikisha unajisajili kwa kubonyeza link hii:👇 https://www.eac.int/juakali-form

Lengo la fomu ya usajili ni kurekodi wasifu wa washiriki pamoja na bidhaa zitakazowasilishwa kwenye maonesho hayo.  

Aidha, taarifa zitakazokusanywa zitatumika kutathmini kiwango cha biashara kilichofanyika, biashara mpya zilizoanzishwa na changamoto mbalimbali ili kuimarisha mazingira ya ujasiriamali kwa MSMEs katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Tunawahimiza wanachama wote wa TWCC kuchangamkia fursa hii muhimu ya kuonyesha bidhaa, kujifunza, kubadilishana uzoefu na kupata mitandao ya kibiashara kimataifa

Ukishajaza hio fomu kwenye link mtumie jina lako kiongozi wa Mkoa/Katibu wa TWCC Mkoani kwako. 

Viongozi wa Mikoa watawasilisha majina makao makuu ya wanachama wote wa TWCC waliojisajili kushiriki maonesho haya kwa hatua nyingine za Kichama. 

Asanteni.  
TWCC Secretariat
0757 823 982 |info@twcc-tz.org