Back to News

TWCC MAONESHO YA 50 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM - SABASABA 2026

1 Apr 2026
TWCC MAONESHO YA 50 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM - SABASABA 2026

Habari njema kwa Wanawake Wajasiriamali Nchini🔥👏 

Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) tunapenda kuwatangazia  Wanachama na Wanawake wote wajasiriamali kutoka Mikoa yote kuwa zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki Maonesho ya 50 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam - Sabasaba 2026 limefunguliwa rasmi

Maonesho yataanza Tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2026

Mahali: Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, Sabasaba Dar es Salaam

 Gharama za ushiriki 
1. Kibanda Cha Mita 9 wanakaa watu 4 (Kila mmoja )ni sh. 250,000 

2. Kibanda cha Mita 9 wanakaa 3 ( kila mmoja) ni Tsh. 350,000 

3. Nusu kibanda ni Tsh. 500,000

 Lipia Kupitia : CRDB Bank
Akaunti: 01J1029021100 
Jina: Tanzania Women Chamber of Commerce

Ukishafanya malipo tafadhali jaza fomu ya ushiriki kupitia link hapa chini 👇👇

https://sabasaba.twcc-tz.org/

Gharama Zitahusisha;
Meza, Kiti🪑, Mapambo, Ulinzi,Umeme, Sare, Mafunzo, Matangazo.

Mwisho wa kuthibitisha na Kulipia : 30 Aprili 2026.

NB: Kila mshiriki atajigharamia kitambulisho, Gharama za Kitambulisho ni Tshs. 30,000/-


 Bidhaa zinazoruhusiwa:  Bidhaa kutoka sekta zote  zinazozalishwa ndani ya nchi, pamoja na teknolojia ndogo ndogo za uongezaji thamani. 

 Kwa Mawasiliano zaidi ; tupigie kupitia namba:0757823982

JISAJILI MAPEMA NAFASI ZIKIJAA DIRISHA LA USAJILI LITAFUNGWA